Aina za sentensi za Kiswahili.

Sentensi huainishwa kuzingatia vigezo mbalimbali.Hapa tutaangazia aina za sentensi kimuundo kama ifuatavyo:

1.Sentensi sahili-Hii ndio sentensi ya kimsingi katika lugha na huwa na kiima na kiarifa kimoja tu.Aidha,husheheni wazo/dhana moja tu.K.m Mtoto anasoma.

2.Sentensi ambatano/ambatani-Hii ni mjumuiko wa vishazi huru viwili.Hapa kuna muungano wa sentensi mbili zenye uzito sawa.Sifa zake ni: huwa na vishazi viwili au zaidi na kuna matumizi ya viunganishi mbalimbali k.v japokuwa,ilhali,minghairi ya,kwa sababu n.k.K.m Muziki unaimba huku watoto wakicheza.

3.Sentensi changamano/changamani-Hii ni sentensi inayosheheni vishazi viwili yaani kishazi huru na tegemezi.Kishazi huru hujisimamia kama sentensi kamili (sentensi sahili) ilhali kishazi tegemezi ni tungo isiyo kamili yaani inategemea kishazi huru ili ikamilike.Kishazi tegemezi pia hutoa habari zaidi kuhusu kishazi huru.K.m Nguo ambazo zilioshwa leo asubihi zitakauka leo jioni.Aghalabu aina ya sentensi hii huwa na matumizi ya amba- rejeshi au O- rejeshi.

Ngeli ya A-WA na muundo wake.

Ngeli hii hutumika sana kwa vitu vilivyo hai mathalan wadudu,wanyama,ndege, binadamu n.k

Ikumbukwe kuwa tunapozungumzia binadamu,tusisahau kuwa atapoaga hivyo kuwa maiti bado anahitaji heshima zake hivyo maiti apo katika hii ngeli.Ni makosa ya kisarifu kusema ‘Maiti ilizikwa’.Ila tunasema ‘Maiti alizikwa.’

Muundo ya ngeli hii inadhihirika kama ifuatavyo:

1.MU k.v katika neno ‘Muumba.’

2.M k.v katika neno ‘Mtu’

3.MW k.v katika neno ‘Mwanafunzi’.

4.KI k.v katika neno ‘kiroboto’

Miundo Ya Silabi Za Kiswahili.

Kuna miundo mbalimbali za silabi za kama ifuatavyo.

1.Silabi za Irabu pekee k.v katika maneno kama vile oa na ua.

2.Silabi za K+I-Hapa ndipo maneno mengi ya Kiswahili yanapatikana.Maneno huwa na silabi moja, mbili au zaidi.Mifano ipo katika maneno kama vile mama,baba n.k

3.Silabi za K+K+I-Konsonanti za mwanzo katika muundo huu huwa na vitamkwa vya ving’ong’o/nazali.Mifano ya maneno ni kama ndevu,Mbacha n.k

4.Silabi za K+k+I-Hapa konsonanti huwa mwanzo kisha kufuatiwa na kiyeyusho na kumalizika kwa irabu.Mifano ya maneno yenye silabi za muundo huu ni kama vile mbwa,mwadhama n.k

5.Silabi za K+K+K+I-Muundo huu hushamiri katika maneno yaliyoswahilishwa/kukopwa kutoka lugha za Kigeni.Mifano ya maneno ni kama vile Skrubu n.k

6.Silabi za K+I+K-Maneno yaliyo na muundo huu ni yale ya kibantu au yaliyokopwa.Silabi funge hushamiri hapa sana.Mifano ya maneno ni kama vile labda, teknolojia n.k

(K inasimamia konsonanti,k inasimamia kiyeyusho (/w/ na /y/),I inasimamia irabu.

Aina Za Silabi.

Silabi ni mpigo mmoja wa sauti.Kuna aina mbili kuu za silabi katika lugha ya Kiswahili.

Aina ya kwanza huitwa silabi huru/wazi.Silabi hii mara nyingi huishia kwa irabu.Sauti za silabi hii husikika kwa nguvu.Mifano ya maneno yenye silabi hii ni kama vile lala,Ndaki, sebule n.k

Ya pili inajulikana kama silabi funge.Hii silabi nayo hishia kwa konsonanti.Mifano ya maneno yenye silabi hii ni maneno yaliyokopwa mathalani labda, alhamisi n.k.

Tofauti kati ya Fonolojia na Fonetiki.

Licha ya kwamba taaluma ya fonolojia na fonetiki hukaribiana sana, kutegemeana na kukamilishana kwa kuwa zote huchunguza sauti, kuna tofauti kadhaa kama zifuatazo.

1.Uchunguzi wa kifonolojia huzingatia mfumo maalum wenye utaratibu fulani ilhali uchambuzi wa kifonetiki.

2.Uchambuzi wa kifonolojia huzionyesha zile sifa bainifu katika lugha mahususi.Kwa upande mwingine taaluma ya fonetiki huorodhesha sauti zote na kutoa ufafanuzi kiumakinifu zinazoonesha tofauti zote za kifonetiki katika foni.

3.Fonolojia huwa nyingi kama idadi ya lugha zilizopo duniani kama vile fonolojia ya kijaluo,kijerumani,kifaransa n.k.Fonetiki nayo huwa moja tu.

4.Fonolojia hushughulikia sifa za kiarudhi zilizo bainifu katika lugha husika na kutupilia mbali zile sifa zisizo bainifu katika lugha inayochunguzwa.

5.Wanafonolojia hukusanya tu sehemu ndogo ya sauti ya lugha fulani ilhali wanafonetiki h sauti nyingi kutoka lugha mbalimbali duniani.

6.Fonolojia huchambua sauti zilizo katika mfumo mmoja na lugha mahususi.Fonetiki huchunguza sauti za lugha kwa ujumla bila kuzingatia sauti hizo zinatumika wapi,vipi na kwa nini.

Tofauti kati ya Fonolojia na Fonetiki.

Licha ya kwamba taaluma ya fonolojia na fonetiki hukaribiana sana, kutegemeana na kukamilishana kwa kuwa zote huchunguza sauti, kuna tofauti kadhaa kama zifuatazo.

1.Uchunguzi wa kifonolojia huzingatia mfumo maalum wenye utaratibu fulani ilhali uchambuzi wa kifonetiki.

2.Uchambuzi wa kifonolojia huzionyesha zile sifa bainifu katika lugha mahususi.Kwa upande mwingine taaluma ya fonetiki huorodhesha sauti zote na kutoa ufafanuzi kiumakinifu zinazoonesha tofauti zote za kifonetiki katika foni.

3.Fonolojia huwa nyingi kama idadi ya lugha zilizopo duniani kama vile fonolojia ya kijaluo,kijerumani,kifaransa n.k.Fonetiki nayo huwa moja tu.

4.Fonolojia hushughulikia sifa za kiarudhi zilizo bainifu katika lugha husika na kutupilia mbali zile sifa zisizo bainifu katika lugha inayochunguzwa.

5.Wanafonolojia hukusanya tu sehemu ndogo ya sauti ya lugha fulani ilhali wanafonetiki h sauti nyingi kutoka lugha mbalimbali duniani.

6.Fonolojia huchambua sauti zilizo katika mfumo mmoja na lugha mahususi.Fonetiki huchunguza sauti za lugha kwa ujumla bila kuzingatia sauti hizo zinatumika wapi,vipi na kwa nini.

Dhana ya Fonolojia.

Fonolojia ni taaluma inayoshughulikia uchambuzi wa mfumo wa sauti zinazotumika katika lugha fulani mahususi.Kiwango hiki cha lugha huchunguza uamilifu wa sauti mahususi zinazotumika katika lugha maalumu.

Kipashio cha chini kabisa cha Fonolojia ni fonimu.Fonimu ni sauti anuwai zinazotumika kuunda maneno katika lugha ya kiswahili.Aidha , kipashio hiki hutumika kutofautisha maneno ya lugha.K.m hapa na haba.

Dhima ya kwanza ya fonolojia ni kueleza na kufafanua mifanyiko mbalimbali ya kifonolojia mathalani namna sauti zinabadilika kutoka sauti moja hadi nyingine hasa tunapojenga maneno tofauti.

Kazi ya pili ni kuonyesha sifa za kiarudhi katika lugha kama vile shadda,toni,kiimbo.

Jukumu la tatu la taaluma hii ni kueleza jinsi sauti za fonimu hufuatana kujenga silabi na maneno yanayokubalika.K.m Maneno ya Kiswahili huanza kwa irabu au konsonanti lakini kila neno sharti likamilike na sauti ya voweli.Yale maneno yanayokopwa huswahilishwa ili kufuata mtindo huu.

Kazi nyingine ya fonolojia ni kuorodhesha fonimu za lugha husika.

Sifa za lugha.

1.Lugha hufuata mpangilio wa vipashio unaleta maana hasa inayofahamika na watumiaji wa lugha husika.Hii ni muhimu ili sentensi yoyote ile iwe na maana.

2.Lugha hujizalisha kwa kuwa hutumia vipashio vyake kuongeza maneno au misamiati mapya.Misamati huweza kupatikana kupitia urudufishaji au unyambulishaji pale ambapo vipashio vinapachikwa kwenye mzizi wa neno.

3.Lugha huambatana na sauti hivyo binadamu hutamka jambo kinywani japokuwa huweza pia kutumia maandishi ili kuwasiliana.

4.Lugha hufuata utaratibu maalum wa jamii husika wanaotumia lugha fulani.Jambo lolote linalotamkwa kinywani haliwezi thibitishwa kuwa lugha kama haijafuata utaratibu unaokubalika na watumiaji wa lugha.K.m Ni kosa la kisarifu katika kiswahili kusema ‘Shuleni kesho tutaenda.’

5.Lugha hufuata misingi ya fonimu.Aghalabu fonimu hutumia kutofautisha maana.

6.Lugha lazima imhusu binadamu kwa kuwa ndicho chombo cha mawasiliano cha mwanadamu.

7.Lugha huchukua misamiati kutoka nyingine (husharabu) ili kuongezea misamiati yake.

JINSI FASIHI SIMULIZI ILIYOCHANGIA UKUAJI WA FASIHI ANDISHI.

Fasihi simulizi imechangia pakubwa kukomaa kwa fasihi Andishi kwa njia zifuatazo.

1.Nyenzo-Fasihi Andishi na Fasihi simulizi zinatumia lugha kama njia ya kupitisha ujumbe.Ikumbukwe kuwa fasihi simulizi ndiyo iliyokuwa ya kwanza kutumia lugha kisha baadaye fasihi Andishi ikaibuka kimaandishi kwa kutumia lugha kiufundi.

2.Fasihi andishi inaendeleza fasihi simulizi kwa kutumia usimulizi katika kazi yake kwa kuna kuna vitabu vya hadithi k.m riwaya zilizoandikwa kwa kutumia mtindo wa ngano.

3.Maudhui na malengo-mambo mengi yaliyoshughulikiwa na Fasihi Andishi yameshajadiliwa na Fasihi simulizi ila tu pana uchangamano wa jamii na kutiliwa pondo kwa maswala mapya.Pia kuna uwiano mkubwa kati ya ujumbe wa fasihi Andishi na simulizi.

4.Fani-ni jinsi msanii anavyowasilisha ujumbe.Fasihi simulizi imechangia kifani k.m nyimbo, wahusika n.k kwa pia hizi hutumika katika fasihi Andishi.

5.Utendaji-Fasihi Andishi huiga utendaji wa fasihi simulizi.K.m Tamthilia huigizwa jukwaani.