Yaliyomo kwenye ripoti ya BBI yafichuliwa.

Jopo la upatanishi BBI linatarajiwa kuweka wazi yaliyomo katika ripoti yake baada ya kuwapokeza kirasmi rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.Inasemekana kuwa janga la Korona ndilo lililosababisha shughuli hiyo kucheleweshwa.

Duru zinasema kuwa imeafikiwa kuwa na waziri mkuu mwenye mamlaka na naibu wake wawili pamoja na rais pia ambaye atakuwa na manaibu wawili.Waziri mkuu anatarajiwa kuchaguliwa na bunge la kitaifa.

Pendekezo jingine ni kuwa na mawaziri watakaoteuliwa kutoka miongoni mwa wageni.

Bado inasubiriwa kuona mengine ambayo yamo kwenye ripoti yenyewe.

Nifundishe wafundishike.

NIFUNDISHE WAFUNDISHIKE

Moyoni siweki koma, imekita ndoto yangu
Ama kweli ninatama, nishaweka roho yangu
Ukufunzi kazi njema, saidia Mungu wangu
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wawe nao marubani, wapae kwenye anga
Waipasi mitihani, wasikose ule unga
Ujinga hapo shuleni, waupige ile chenga
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wakafike Marekani, waitwe nao wasomi
Wazunguke uzunguni, wazishike zao ndimi
Warudi hapa melini, wasalimu hata nami
Ndoto yangu ukufunzi fundishe wafundishike

Uandishi waushike, kazi yao iwe bora
Kwa riwaya wasifike, mashairi yawe bora
Yamkini watajike, kama yule Walibora
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Natamani watajike, ili nami nitajike
Huko mbali wakafike, mimi naye nisifike
Pale pote wakumbuke, niliwapa hiyo fuke
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

(Akongo Kevin-Malenga)

Nifundishe wafundishike.

NIFUNDISHE WAFUNDISHIKE

Moyoni siweki koma, imekita ndoto yangu
Ama kweli ninatama, nishaweka roho yangu
Ukufunzi kazi njema, saidia Mungu wangu
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wawe nao marubani, wapae kwenye anga
Waipasi mitihani, wasikose ule unga
Ujinga hapo shuleni, waupige ile chenga
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Wakafike Marekani, waitwe nao wasomi
Wazunguke uzunguni, wazishike zao ndimi
Warudi hapa melini, wasalimu hata nami
Ndoto yangu ukufunzi fundishe wafundishike

Uandishi waushike, kazi yao iwe bora
Kwa riwaya wasifike, mashairi yawe bora
Yamkini watajike, kama yule Walibora
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

Natamani watajike, ili nami nitajike
Huko mbali wakafike, mimi naye nisifike
Pale pote wakumbuke, niliwapa hiyo fuke
Ndoto yangu ukufunzi, fundishe wafundishike

(Akongo Kevin-Malenga)

Nahau na maana zake

1.Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka.
mingi
2,Ana mkono wa birika=mtu mchoyo
3.Ametutupa mkono=amefariki,amekufa
4.Ameaga dunia=amekufa,amefariki
5.Amevaa miwani=amelewa
6.Amepiga kite=amependeza
7.Amepata jiko=kaoa
8.Amefumgapinguzamaisha=ameolewa
9.Anawalanda wazazi wake=
kawafanana wazazi wake kwa sura
10.Kawachukua wazazi wake=anafanana
na wazazi wake kwa sura na tabia.
11.Kawabeba wazazi wake=anawajali na
kuwatunza wazazi wake.
12.Chemshabongo=fikiri kwa makini na
haraka.
13.Amekuwa toinyo=hanapua.
14.Amekuwa popo=amekuwa kigeugeu
15.Ahadi ni deni=timiza ahadi yako
16.Amewachukua wazee wake=
anawatunza vizuri wazazi
17.Amekuwa mwalimu=yu msemaji sana
18.Amemwaga unga=amefukuzwa kazi 19..Anaulimuwaupanga=anamaneno
makali
20.Ameongeza unga=mepandacheo
21.Agiziarisasi=pigarisasi
22.Kuchungulia kaburi=kunusurika kifo
23..Fyatamkia=nyamaza kimya
24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana
alama za mapigo ya fimbo mgongoni
25.Hamadi kibindoni=akibailiyopo
mkononi]
26.Hawapikiki chungu
kimoja=hawapatani kamwe
27.Kupika majungu=kumteta mtu kwa
siri
28.Kumvika mtu kilemba cha ukoka=
umsifu mtu kwa unafiki
29Kula mlungula/kula rushwa=kupokea
rushwa
30.Kupelekwa miyomboni=kutiwa au
kupelekwa jandoni
31.Kujipalia mkaa=ujitia matatani
32.Kumeza au kumezzea mate=utamani
33.Kumuuma mtu sikio=kumnong’oneza
mtu jambo la siri
34.Kumpanyamaya ulimi=
kumdanganya mtu kwa maneno

Umalenga ni basi.

UMALENGA NI BASI
Moyo wangu umegoma, kutunga tena sidhani
Ushairi nauhama, malenga sina thamani
Bongo nalo limekwama, tungo hawazitamani
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Yani kote makundini, tungo zangu hazisomwi
Hata kule ulingoni, japo ya mbwa siamwi
Kule kwetu kisimani, naliwa na langu zimwi
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Mzee mpenda watu, hanioni mie kwani
Nazimaliza sapatu, kumfata kikashani
Kwake sisikiki katu, hanipi ‘ta tumaini
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Yule mhindi wa pwani, makundini simuoni
Hivi yuwapi jamani, Raneti aniauni
Azitupe ‘ko hewani, nisikike redioni
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Wenzangu magazetini, tungo zao zapepea
Taifa leo nyumbani, kila wiki watokea
Mwatumia mbinu gani, tungo zenu kutokea
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Huku wengine diwani, tungo zao zachapishwa
Kina Nuhu runingani, wanatamba bila rushwa
Navuma mitandaoni, vimoji vyarushwarushwa
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Pengine mnipe mada, niwaandikie wenza
Nisijezipata shida, mie bado najifunza
Nyumbani ninao muda, hivi kipi chaniponza
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Kama mie nina hila, nifunzeni si mjuzi
Au kama ni Kabila, siwezi pinga Mwenyezi
Kuwalipa sina hela, nawambia waziwazi
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki

Nawaaga kwaherini, nimechoka kulalama
Najitupa muzikini, nikazicheze ‘zo ngoma
Nitatoka makundini, msiambe sijasema
Naitupa mishororo, bora nifanye muziki.

(Daniel Wambua-Malenga)

Visawe na maana zake.

Visawe ni maneno yenye maana sawa.

*Neno=Kisawe*
1. Ardhi=Dunia
2.Ari=Nia
3.Aibu=Soni
4.Azma=Makusudio
5.Binti=Msichana
6.Chakula=Mlo
7.Chanzo=Sababu
8.Cheti=Hati
9.Chuana=Shindana
10.Chubua=Chuna
11.Chubuko=Jeraha
12.Chumvi=Munyu
13.Duara=Mviringo
14.Dunia=Ulimwengu
15.Familia=Kaya
16.Fedha=Hela/Pesa
17.Fukara=Maskini
18.Gari Moshi=Treni
19.Ghasia=Fujo
20.Ghiliba=Hila
21.Godoro=Tandiko
22.Hitimaye=Mwishowe
23.Herufi=Hati
24.Hesabu=Hisabati
25.Hodari=Bingwa
26.Idhini=Ruhusa
27.Jogoo=Jimbi
28.Jokofu=Friji
29.Kandanda=Soka
30.Kenda=Tisa
31.Kichaa=Mwendawazimu
32.Kileo=Pombe
33.Kimada=Hawara
34.Kiranja=Kiongozi
35.Kivumbi=Fujo
36.Kopoa=Zaa
37.Kongoro=Gema
38.Labda=Huenda
39.Labeka!=Abee!/Naam!
40.Laghai=Danganya
41.Lisanj=Ulimi
42.Majira=Wakati
43.Manii=Shahawa
44.Masalia=Mabaki
45.Mashaka=Tabu
46.Mbio=Kasi
47.Mchoyo=Bahili
48.Mdomo=Kinywa
49.Mlolongo=Foleni
50.Motokaa=Gari
51.Msimu=Majira
52.Mtima=Moyo
53.Mtindi=Maziwa Mgando
54.Mtindo=Staili
55.Mtu=Binadamu
56.Muda=Wakati
57.Mvuli=Mvulana
58.Nahodha=Kapteni
59.Nakshi=Urembo
60.Ndoa=Chuo
61.Ndondi=Masumbwi
62.Ndovu=Tembo
63.Nguo=Mavazi
64.Nguzo=Kanuni
65.Nia=Lengo
66.Nuru=Mng’ao
67.Nyanya=Bibi
68.Nyati=Mbogo
69.Ongea=Sema/Zungumza
70.Pombe=Mtindi
71.Raba=Kifutio
72.Rabana=Mola
73.Rafiki=Sahibu/Swahibu
74.Rehani=Poni
75.Rubani=Kapteni
76.Rundika=Tufika
77.Rushwa=Hongo
78.Saka=Winda
79.Sala=Dua
80.Samani=Fanicha
81.Shika=Kamata
82.Shujaa=Jasiri
83.Spika=Kipaza sauti
84.Starehe=Tamasha
85.Sura=Uso
86.Tafrija=Sherehe
87.Terevisheni=Runinga
88.Thenashara=Kumi na mbili
89.Tumbiri=Ngedere
90.Ugonjwa=Maradhi
91.Uja=Ubinadamu
92.Ukaidi=Ujeuri
93.Ukumbi=Surua
94.Ukuta=Kiambaza
95.Ukwasi=Utajiri
96.Upara=Kidazi
97.Urembo=Umaridadi
98.Vamio=Shambulio
99.Vifijo=Vigelegele
100.Vunja=Pasua
101.Vurugu=Fujo
102.Vuu=Ghafla
103.Nyema=Vizuri
104.Wajihi=Uso
105.Wakala=Ajenti
106.Waraka=Barua
107.Waza=Fikiri
108.Weupe=Mwangaza
109.Weusi=Giza
110.Wiki=Juma
111.Winda=Nepi
112.Wivu=Husuda
113.Chupi=Kocho
114.Karai=Beseni/Dishi
115.Mamba=Kenge.

Magatuzi yatakayomfanya Ruto awe rais mwaka wa 2022.

Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 tayari imeanza huku wanasiasa tofauti waliokimezea mate kiti cha urais wakienda kaunti mbalimbali kutafuta uungwaji mkono.

Naibu wa rais, William Ruto amekuwa kwenye ziara katika kaunti ya Kisii na Kajiado ambapo umati mkubwa ulijitokeza kuhudhuria mkutano wake.Hii ni ishara tosha kuwa ana ufuasi kutoka kwa wananchi.

Baadhi ya kaunti ambazo huenda akapata kura nyingi kwenye uchaguzi ujao ni zile zinapatikana kwenye eneo la bonde la ufa,machakos,makueni, Kakamega na Nyamira.

Wasomi nchini nafasi zenu ni nini?

Salamu ziloyakini, wajumbe tusikizeni,
Tubebazo kwa makini, tunataka wajuzeni,
Mengi tumeyabaini, nanyi tuwaulizeni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Umma wawasubirini, toka huko mitaani
Asilimia tisini, watetezi mu njiani,
Vipi hamujiamini, na kujishusha thamani,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Enyi wasomi nchini, nawaeleza bayani,
Tuikamateni dini, tuepuke ushetani,
Hapo tutajaaini, na kujua kiundani,
Kwamba wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jamii inatamani, ile elimu auni,
Kuondolewa gizani, kuepuka hali duni,
Tusiwepo mashakani, mutupunguze huzuni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jama! tuelimisheni, watu waache uhuni,
Dhima tuiepukeni, tusije kufanywa kuni,
Dini tulinganieni, yasije ya filauni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Jamani jitambueni, muwapo kule Ndakini,
Eti Bweni kiumeni, dada anafata nini,
Au bweni la kikeni, dume lakaa kitini,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini?

Kaditama ukingoni, nudhumu yangu mwishoni,
Wasomi toka vyuoni, kwetu ninyi ndio mboni,
Ujumbe pasi na soni, wa anuani tungoni,
Enyi wasomi nchini, nafasi zenu ni nini

(Mtunzi: Abdallah Hanga)

Mwenye kupaka midomo.

Nauliza si utani,wala sizuwi fitina
Naomba jibu wendani,lenye kina na maana
Hii rangi midomoni,huwa ina ma’na gani?
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Mahaba mnatatiza,mabinti wa siku hizi
Nyoyo mnatuumiza,kisi sasa hatuwezi
Midomo mnashangaza,walahi mwatupa kazi
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Rangi hii midomoni,nyengine hasa ni sumu
Haina raha jamani,mapenzi kukosa hamu
Mwatunyanyasa wendani,kisha na kutudhulumu
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Majike mloolewa,lengo lenu huwa gani?
Kikweli mwajiumbuwa,hamvutii jamani
Na yule ulochumbiwa,kisi upigwaje hani?
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Dume fulani majuzi,lilisaka sidechiki
Kapigwa kisi mjuzi,penzi na yake mikiki
Kurudi nyumbani mwizi,akajulikana haki!
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Rangi zilitapakaa,midomo na lake shati
Ilivyozuka balaa,tafurani hatihati
Kisha mwisho wa fadhaa,ikachanwa ndoa cheti
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Rangi zina ma’na gani,iwapo mnapendana
Mwalimu sasa sioni,wala situkui dhana
Mpunguzeni jamani,rangi haina maana
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi?

Sitaki kusema sana,hapa mwalimu nakoma
Nipeni jibu la ma’na,liridhishalo mtima
Nawangoja waungwana,naomba fanyeni hima
Mwenye kupaka midomo,hasa apigwaje kisi.

(Mwalimu Baxtone)

Nani atakua mgombea mwenza wa Raila 2022.

Huku kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022 zikiwa zimeanza kushika kasi,watu wengi bado hawafahamu iwapo kiongozi wa upinzani Raila Odinga atawania kiti cha urais.Licha ya sintofahamu hiyo,ishara zaonyesha kuwa atakuwa debeni.Swali sasa ni kuwa ni nani ambaye atakuwa mgombea mwenza wake?

Kumekuwa na wanasiasa wengi ambao wanaonekana kuwa huenda wakachukua wadhfa huo wa kuwa mgombea mwenza.Miongoni mwao ni gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, gavana wa kakamega Wickliyffe Oparanya, waziri wa maswala ya ndani Fred Matiangi,Anne Waiguru,Gideon Moi na wengineo.

Gideon Moi ana nafasi kubwa kwa sababu ufuasi wake katika maeneo ya bonde la ufa utawezesha kuwagawanya kura hivyo kumtoa kijasho William Ruto.

Joho ana ufuasi mkubwa kutoka eneo la Pwani na hata sasa hivi ndiye kigogo wa eneo hilo.Aidha, yeye pia ni naibu mwenyekiti wa chama cha ODM.

Waiguru naye kwa upande mwingine ndiye anayetazamiwa kuwa kigogo wa eneo la kati baada ya rais Kenyatta kutoka mamlakani.

Oparanya naye anaonekana kumpa ushindani kiongozi wa ANC,Musalia Mudavadi katika eneo la magharibi hivyo kura nyingi zitatoka huko.