Vyuo vikuu vya kibinafsi vilivyo bora nchini Kenya.

Kwa muda sasa taasisi za juu ya elimu nchini Kenya zimekumbwa na changamoto si haba kuhusiana na ubora wa mafunzo wazo.Kwenye upeo wa kimataifa vyuo vikuu vya umma vimeshamiri kulingana na takwimu zinatolewa kila uchao.Licha ya takwimu hizi baadhi ya vyuo vikuu vya kibinafsi pia zimeonekana zikitia fora.

Baadhi ya vyuo vikuu vya kibinafsi zilizo bora nchini Kenya ni kama vifuatavyo.

1.Chuo cha East African Baraton

Chuo hichi kilianzishwa mwaka wa 1978 kama shule ya kiadventista.Kipo mjini Eldoret na Nairobi.

2.Chuo cha Strathmore.

Chuo hiki kilianzishwa mwaka 2002.Kipo mjini Nairobi.

3.Catholic University of East Africa.

Hichi nacho kilianzishwa mwaka 1989.Kinapatikana mjini Eldoret, Nairobi na Kisumu.

4.United States International University of Africa.

Hiki chuo kilianza kufanya kazi nchini Kenya mwaka 1989.Kina tawi lake Nairobi.

5.Mount Kenya University.

Hiki chuo kilianzishwa mwaka 2008.Ni mojawapo kati ya vyuo vinavyojulikana sana nchini Kenya.Kina tawi Nakuru, Nairobi,Kitale.

Yaliyomo kwenye ripoti ya BBI yafichuliwa.

Jopo la upatanishi BBI linatarajiwa kuweka wazi yaliyomo katika ripoti yake baada ya kuwapokeza kirasmi rais Kenyatta na kiongozi wa upinzani Raila Odinga.Inasemekana kuwa janga la Korona ndilo lililosababisha shughuli hiyo kucheleweshwa.

Duru zinasema kuwa imeafikiwa kuwa na waziri mkuu mwenye mamlaka na naibu wake wawili pamoja na rais pia ambaye atakuwa na manaibu wawili.Waziri mkuu anatarajiwa kuchaguliwa na bunge la kitaifa.

Pendekezo jingine ni kuwa na mawaziri watakaoteuliwa kutoka miongoni mwa wageni.

Bado inasubiriwa kuona mengine ambayo yamo kwenye ripoti yenyewe.

Magatuzi yatakayomfanya Ruto awe rais mwaka wa 2022.

Kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022 tayari imeanza huku wanasiasa tofauti waliokimezea mate kiti cha urais wakienda kaunti mbalimbali kutafuta uungwaji mkono.

Naibu wa rais, William Ruto amekuwa kwenye ziara katika kaunti ya Kisii na Kajiado ambapo umati mkubwa ulijitokeza kuhudhuria mkutano wake.Hii ni ishara tosha kuwa ana ufuasi kutoka kwa wananchi.

Baadhi ya kaunti ambazo huenda akapata kura nyingi kwenye uchaguzi ujao ni zile zinapatikana kwenye eneo la bonde la ufa,machakos,makueni, Kakamega na Nyamira.

Nani atakua mgombea mwenza wa Raila 2022.

Huku kampeni za uchaguzi wa mwaka 2022 zikiwa zimeanza kushika kasi,watu wengi bado hawafahamu iwapo kiongozi wa upinzani Raila Odinga atawania kiti cha urais.Licha ya sintofahamu hiyo,ishara zaonyesha kuwa atakuwa debeni.Swali sasa ni kuwa ni nani ambaye atakuwa mgombea mwenza wake?

Kumekuwa na wanasiasa wengi ambao wanaonekana kuwa huenda wakachukua wadhfa huo wa kuwa mgombea mwenza.Miongoni mwao ni gavana wa Mombasa Ali Hassan Joho, gavana wa kakamega Wickliyffe Oparanya, waziri wa maswala ya ndani Fred Matiangi,Anne Waiguru,Gideon Moi na wengineo.

Gideon Moi ana nafasi kubwa kwa sababu ufuasi wake katika maeneo ya bonde la ufa utawezesha kuwagawanya kura hivyo kumtoa kijasho William Ruto.

Joho ana ufuasi mkubwa kutoka eneo la Pwani na hata sasa hivi ndiye kigogo wa eneo hilo.Aidha, yeye pia ni naibu mwenyekiti wa chama cha ODM.

Waiguru naye kwa upande mwingine ndiye anayetazamiwa kuwa kigogo wa eneo la kati baada ya rais Kenyatta kutoka mamlakani.

Oparanya naye anaonekana kumpa ushindani kiongozi wa ANC,Musalia Mudavadi katika eneo la magharibi hivyo kura nyingi zitatoka huko.

Sababu ya Murathe kuunga mkono Raila awe Rais.

Naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee David Murathe amesema mara si moja kuwa haungi mkono Ruto awe rais 2022 na badala yake anapigia upato Raila kuwa rais.Akihojiwa na gazeti la Standard, Murathe amedai kuwa makabila mawili tu ndio yamekuwa yakiongoza Kenya hivyo ni vema mwaka 2022 rais atoke katika kabila tofauti.Alisema Raila ana historia nzuri ya kutetea demokrasia nchini Kenya hivyo ingekuwa vizuri kama wakenya wangempa angalau muhula mmoja ahudumu kama Raila.Murathe pia amesema hana tatizo lolote na Ruto ila yeye haifai kuwa rais sababu yumo ndani ya makabila hayo mawili.

Aidha, alisema kuwa Raila akimaliza hatamu ya uongozi ndipo sasa anaweza wachia vijana uongozi.Matamshi yake yanakuja siku chache baada ya kusema hakuna yule anaweza kuwa rais baada ya Kenyatta kumaliza muhula wake isipokuwa Raila.

Jinsi Raila atamshinda Ruto 2022.

Kiongozi wa ODM, Raila Odinga na naibu wa rais, William Ruto wameonakana kuwa mahasimu hivi karibuni kutokana na uchaguzi unaokaribia 2022.Wote wameonakana wakipiga kampeni za mapema kutafuta wafuasi.Yasemekana Raila atajitosa kinyang’anyironi kwa mara ya tano baada ya kushindwa mara nne kwenye uchaguzi wa urais.Ingawa kiongozi huyo wa upinzani amekwepa mara si moja kutangaza azma yake ya kuwania urais mwaka wa 2022,ishara zote zaonyesha kuwa atakuwa debeni kwenye uchaguzi ujao.Ikumbukwe kuwa Ruto alijifunza mengi alipokuwa kwenye chama cha ODM na kujua siasa anazopenda Raila hivyo kumpa ushindani mkubwa.Huenda Raila akapata kura nyingi kwenye kaunti kama vile Mombasa,Kisumu,Taita Taveta,Kitui,Makueni,Migori, Homabay,Kisii, Nairobi na zinginezo.Hii ni licha ya kugura kwa wanasiasa kadhaa kama vile Johsone Muthama,Boni Khalwale,Hassan Omar;wote ambao walikuwa katika mrengo wa NASA.Raila pia amepata uungwaji mkono kutoka kwa naibu mwenyekiti wa chama cha Jubilee,David Murathe

Maseneta waafikiana kuhusu mfumo wa ugavi wa mapato.

Hatimaye mzozo wa mfumo wa ugavi wa mapato umepata suluhu ya kudumu baada ya maseneta kuafikiana kuhusu mfumo uliopendekezwa na kamati ilichaguliwa kutafuta suluhu.Kamati hiyo inaongozwa na seneta wa Bungoma Moses Wetangula na mwenzake wa Nairobi ilikubaliana kuwa hakuna kaunti itapoteza fedha kutokana na mfumo huo mpya.

Ikumbukwe maseneta walikosa kupitisha miswada kadhaa na hivyo kuangushwa mara tisa kabla ya Rais Kenyatta na kiongozi wa ODM kuingilia kati.Viongozi hao wawili waliongoza mkutano siku ya Jumanne kutafuta suluhu.

Suluhisho hili linakuja siku moja baada ya magavana kusitisha huduma kwenye gatuzi zao kutokana na ukosefu wa fedha.

Raila akiri Ruto ni tishio 2022.

Kiongozi wa upinzani,Raila Odinga amesema wazi kuwa Ruto ni tishio kubwa 2022 kisa na maana ameshajipendekeza kwa vijana.Naibu wa Rais ameonakana kupendwa na vijana na kupata ufuasi mkubwa kutokana na juhudi zake za kuwakwamua kiuchumi.Amekuwa akiwapa vijana toroli na bidhaa zingine nyingi jambo ambalo limemkera kiongozi wa ODM.

Hivi majuzi kwenye mkutano wa kupigia debe ripoti ya jopo la upatanishi (BBI) katika gatuzi la Taita Taveta, alidai Ruto ana nia ya kufurahisha tu vijana ila wampe kura kisha awageuke.Alisema Ruto amekuwa serikalini tangu mwaka 2013 ilhali hakuna alichofanya kuinua uchumi wa vijana na hivyo hamna lolote la kufanya sasa

Naibu wa Rais,Dr.Ruto akiri kufukuzwa kwenye makao ya Mombasa.

Naibu wa rais,Dr.Ruto amekiri siku ya jumapili pili kuwa alitimuliwa kutoka makao yake ya Mombasa pamona na mkewe.Mwaka uliopita, Desemba,Ruto alifukuzwa na baadhi ya waliosema kuwa walipata amri kutoka juu.

Ruto alidai kuwa kuna baadhi ya watu wanaofikirika kushirikiana na upinzani ili kuhujumu utendakazi wake.Alisema wanatumia mbinu zote kuzua rabsha katika yake na Rais Kenyatta.

Ruto alisema kuwa anajua mipango yao na hatajiingiza kwenye mtego uliowekwa nao ili kutofautiana na rais kwenye umma.Ikumbukwe kuwa siku za hivi karibuni,naibu wa rais amekumbwa na misukosuko kuhusu mstakabali wake wa kisiasa baada ya wandani wake kulalamika kuwa anahujumiwa na rais.Kauli hii inatokana na Kipchumba Murkomen.

Waziri Mutahi Kagwe akana kuhusika kwenye kashfa ya KEMSA.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amekana kuhusika katika sakata ya shirika la usambazaji dawa la KEMSA.Kwenye mahojiano na kamati ya afya katika bunge, alisema kuwa madai yaliyotolewa na afisa mkuu mtendaji wa KEMSA hayana msingi.

Ikumbukwe kwamba Jona Manjari wiki jana alidai kuwa Kagwe aliyekuwa akitoa amri ya nani kupatiwa tenda ya kusambaza vifaa vya kujikinga dhidi ya Korona kupitia jumbe za simu.Kagwe alisema kuwa ana wajibu wa kushikiniza yeyote chini ya wizara yake kufanya kazi ili manufaa yajitokeze lakini hakuhusika katika kufanya maamuzi ya ununuzi wa vifaa vya kujikinga dhidi ya Korona.Aidha Kagwe pia alikana kuhusika katika biashara yoyote na shirika hilo.

Sasa inatazamiwa kuona jinsi tume ya maadili na kupana na ufisadi (EACC) itakayoshughulikia swala hilo la ubadhirifu wa fedha za kupana na Korona baada ya kupatiwa makataa ya siku thelathini na Rais Kenyatta ikishindikana na tume nyingine.Kashfa hii ilijitokeza wazi baada ya ufichuzi wa kituo cha televisheni cha NTV kwenye makala ya COVID-19 billionaires yaliyopeperushwa siku chache zilizopita.