Vikwazo vya maenezi ya Kiswahili katika enzi ya ukoloni.

Ingawa lugha ya Kiswahili ilienea sana, lakini kulibainika vilivile vikwazo vilivyo
tatiza maenezi yake, Japo Kiswahili kilikuwa kimeenea mataifa mengi Afrika
Mashariki lakini kuna vikwazo vingi vilivyoifanya lugha hii kutopiga hatua kwa
mataifa mengineo ya Afrika na lau sivikwazo hivyo Kiswahili kungekuwa lugha
ya mataifa mengi ya bara Afrika, miongoni mwa sababu hizo:
1- Dharau za Wazungu kwa Waafrika
Mfumo wa utawala wa Wazungu na Waingereza, ulileta pingamizi kubwa katika
maenezi ya Kiswahili. Waingereza waliwadharau sana Waafrika na mambo yao
yote kukiwemo lugha zao. Kiswahili kama mojawapo ya Lugha za Kiafrika
haingeweza kuepuka dharau hizo.
Kwa upande mwengine Wakoloni walichukulia kuwa lugha yao ya Kiengreza ni
adhimu na yenye manufaa kuliko lugha yeyote, na mwenye kutaka ustaarabu
lazima ajifunze Kiingereza, waliweza kukuza lumbikizo hizo kwa kupitia mashule
walioazisha na nafasi za kazi ambazo waliwapa kipawa mbele wanaojuwa Kiingereza, pia waliweka mawazo kwenye akili za watu kuwa Kiswahili hakitoshi
kunfanya mtu astaarabike.
Kwa sababu hizo za chuki Waaingereza walianzisha lugha rasmi za matumizi kwa
Mwafrika, hivyo basi Kiingereza kikapawa hadhi kubwa na ya juu kufanywa
lugha rasmi kisha Kiswahili. Hapo basi Kiingereza kikawa ndio lugha ya
Ustaarabu na yeyote aliyetaka kustaarabika alijifunza Kiingereza.
Kuna fikra mbaya zaidi iliyoenezwa na Wazungu hao, nao nikuwa Kiswahili
hakina misamiati yakuendesha shughuli za kielimu na taaluma isipokuwa
Kiingereza kwa maoni yao Waafrika ni watu washenzi na washamba.
Mawazo hayo yaaliwaathiri sana wenyeji na wengi wakaanza kuutoroka Uafrika
tamaduni na hata lugha, na wengi wakaanza kutafuta ustaarabu katika lugha za
kigeni. Kwa mfano Kenya na Uganda, kuna baadhi ya viongozi hadi leo waamini
kuwa kiingreza ni bora kuliko Kiswahili na lugha nyengine za Afrika.
2- Kiswahili ni lugha geni.
Kuna baadhi ya watu walidai kuwa Kiswahili ni lugha geni yaani ni Kiarabu,
nahivyo basi kilikuwa hakina nafasi hapa Africa Mashariki na yakati. Hivyo basi
wakaonelea ni heri wajifunze lugha za kienyeji badali ya Kiarabu, tume ya Philips
stoke ya 1924, nchini Kenya ilipendekeza matumizi ya lugha ya Kikamba, Kijaluo,
Kikikuyu, na Kiluhya, nchini Uganda walipendekeza Kiingereza na Luganda,
katika maeneo ya kifalme na hata maeneo yasiokuwa ya kimalme, nchini Zaire
Waluba, Wakongo na Walingala walikataa katakata kusanifishwa kwa Kiswahili
cha Kiungwana kwa sababu walidai kuwa ni lugha geni ya Afrika Mashariki na
basi haina nafasi Zaire ndiposa Kifaransa kikaendelezwa na Wabelgiji.
3- Dhana kwambaKiswahili kiliendeleza Uislamu.
Nao Wamishonari hawakukipenda Kiswahili kwa madai yakuwa Kiswahili
chaendelza Uislamu ilihali wao walitaka kuendeleza Ukiristo, hali hiyo
iliwapelekea kukusanifisha Kiswahili wakidai kuwa walikuwa wakiondoa Uarabu
na Uislamu katika Kiswahili, pia walidai wataka kukipa chombo cha kueneza dini
ya Ukiristi nidhamu, haya yote yalifanywa na Wameshinari wakishirikiana na Wazungu kwakutambua hakuna lugha nyengine yaweza tumiwa kwa mambo ya
Mungu isipokuwa Kiswahili.
Kwa mtazamo wa makini twaweza sema lau Wakoloni na Wamishonari
wangekuwa na lugha mbadala kuliko Kiswahili basi wamgetumia lugha hiyo na
wangeiacha lugha ya Kiswahili, lakini kwa kuwa ingekuwa gharama kufasiri
baadhi ya vitabu vyao kama Biblia katika lugha nyengine za Kiafrika basi
waliazimia kutumia Kiswahili, nchini Uganda na Kenya kuna tume ziliochaguliwa
kuchunguza matumizi ya Kiswahili kwakuwa lugha hii imekabiliana na Uislamu.
4- Biashara.
Kwa jumla biashara ni miongoni mwa viekezo vikuu vilivyoifanya lugha ya
Kiswahili kuenea Afrika Mashariki, ingawa hivyo biashara hii ilitumiwa na
Wakoloni kuifanya lugha ya Kiswahili kuchukiwa na kuonekana lugha mbaya.
Waingereza walieneza propaganda kuwa Kiswahili na wanaotumia Kiswahili
wamefungamana na biashara ya watumwa, nayo fikira ikaeneya kwa jamii kwani
biashara ya watumwa ilikuwa ni biashara mbaya na yeyote aliyetoka maeneo ya
bara alimchukia mwenye kufanya biashara hiyo nakumuona adui, kwahivyo
Kiswahili kikachukiwa na Waswahili wenyewe wakachukiwa kwa kuhusishwa na
biashara ambazo hazikuwa za kweli.
Kawaida biashara siku zote huhusishwa na porojo na ukora na ujanja mwingi, basi
ikawa lugha ya Kiswahili ni lugha ya wakora na wajanja wenye kufanya biashra za
watumwa, kwa sababu hizo lugha hii ikawa wengi katika wageni hasa wasiotoka
maeneo ya mwambao waichukia.

(Makala haya ni kwa hisani ya DR.K.M Kame)

Matatizo yanayoikumba lugha ya Kiswahili.

Licha ya kuwa lugha ya Kiswahili imepiga hatua kubwa bado kuna changamoto si haba katika kuikuza.

Baadhi ya changamoto hizo ni pamoja na yafuatayo.

Kwanza,lugha hii imepata upinzani mkubwa kutoka kwa lugha nyingine kama vile Kiingereza, Kifaransa,Kijerumani, Kiarabu n.k

Pili,kuna dhana kuwa Kiswahili ni lugha ya watu duni hivyo kutengwa katika matumizi katika nyanja mbalimbali.

Tatu,pana ukosefu wa sera maalum ya matumizi ya lugha ya Kiswahili katika nchi kadhaa kama vile Kenya.

Nne,kuna ukosefu wa walimu wa wakutosha wakufunza lugha ya Kiswahili waliohitimu.

Aidha,kuna kudharauliwa kwa lugha ya Kiswahili na kupigiwa chapuo kwa lugha za kigeni.

Itikadi za Waswahili.

Waswahili wana itikadi nyingi sana.

Itikadi ni taasisi iliyo hai katika tamaduni za jamii zote za wanadamu.

Ushirikina ni sehemu ndogo ya itikadi za watu.Uislamu na Ukristo haufunzi wa kuhimiza itikadi za ushirikina.Lakini baadhi ya waumini hujikuta wamejaa tele ndani ya uwanja huu wa maisha.

Itikadi za waswahili wa mwambao wa Kenya ni pamoja na imani ya kuwepo pepo majini, mashetani n.k nguvu na uwezo wa pepo hao katika kulinda mashamba,mali,miji, kusaidia kutibu maradhi.

Pamoja nazo Waswahili wana mila kama vile miiko mbalimbali.Kwa mfano kula gizani ni kula na shetani, kunywa maji msalani ni mwongo,bundi akilia juu ya nyumba anatangaza kifo.

Kuna hitma ya mji, Waswahili huushuka fuoni wakatinda (wakachinja) ng’ombe na kula hukohuko na baadaye mifupa kutiwa kapuni na kuenda kutupwa bahari kuu.Hufanya hivi kwa itikadi ya kusafisha mji na kuweka mbali na taabu na huzuni za kilimwengu.Itikadi zina mafunzo mengi yanayostahili kuhifadhiwa na kuzingatiwa.

Ndoa na harusi za Waswahili.

Uswahilini,ndoa na harusi ni taasisi ya kwanza kwa uzito wa maisha ya kila siku ya mtu.

Ubikira ni ada kubwa sana kwa wasichana waswahili kabla ya kuolewa kwani ndoa ndicho kitovu cha maisha ya waswahili.

Huwa ni desturi iliyoenea mwote uswahilini wa wazazi na mashangazi kuwa washauri wakuu wa ndoa za watoto wao.

Kuna hatua kadhaa tangu mtu aposapo hadi kutoa mahari na kufunga ndoa.Chuo hicho ndicho huwashirikisha makungwi na masomo katika kuwaelekeza na kuwafundisha wari harusi kabla na baada ya harusi.

Kwa waumini wa kweli wa Uislamu sheria za kiislamu huwa na ndicho kigezo pekee chakuendesha maisha ya ndoa.

Mazishi ya Waswahili.

Mazishi ni taasisi ya kuwarejesha waja walikotoka ama na kuwakumbusha walio hai juu ya marejeo hayo kwa Mola wao.

Msiba wa kifiliwa huwa ni faradhi-kifaya (faradhi ya kutosheleza).Kufiliwa huwa ni kazi kwa wote na kazi kubwa kwa majirani na marafiki ni kuwafariji jamaa ya waliofiwa.

Kazi zote kuanzia uchimbaji kaburi, kupatikana kwa tusi, uchukuaji wa jeneza,uzikaji wa maiti na swala zote za kumsalia maiti ni za jumuiya.

Maiti huoshwa na watu wake wa karibu na hapo ndipo utajua jamaa wa karibu wa marehemu kwani huyo ndiye ataingia jofuni.Huzuni ya kifo,kwa msingi huchukua ada ndogo ndogo za dua na kufagilia mavani kila mwaka daima.

Mazishi ya Waswahili.

Mazishi ni taasisi ya kuwarejesha waja walikotoka ama na kuwakumbusha walio hai juu ya marejeo hayo kwa Mola wao.

Msiba wa kifiliwa huwa ni faradhi-kifaya (faradhi ya kutosheleza).Kufiliwa huwa ni kazi kwa wote na kazi kubwa kwa majirani na marafiki ni kuwafariji jamaa ya waliofiwa.

Kazi zote kuanzia uchimbaji kaburi, kupatikana kwa tusi, uchukuaji wa jeneza,uzikaji wa maiti na swala zote za kumsalia maiti ni za jumuiya.

Maiti huoshwa na watu wake wa karibu na hapo ndipo utajua jamaa wa karibu wa marehemu kwani huyo ndiye ataingia jofuni.Huzuni ya kifo,kwa msingi huchukua ada ndogo ndogo za dua na kufagilia mavani kila mwaka daima.

Nahau na maana zake

1.Amekula chumvi nyingi=ameishi miaka.
mingi
2,Ana mkono wa birika=mtu mchoyo
3.Ametutupa mkono=amefariki,amekufa
4.Ameaga dunia=amekufa,amefariki
5.Amevaa miwani=amelewa
6.Amepiga kite=amependeza
7.Amepata jiko=kaoa
8.Amefumgapinguzamaisha=ameolewa
9.Anawalanda wazazi wake=
kawafanana wazazi wake kwa sura
10.Kawachukua wazazi wake=anafanana
na wazazi wake kwa sura na tabia.
11.Kawabeba wazazi wake=anawajali na
kuwatunza wazazi wake.
12.Chemshabongo=fikiri kwa makini na
haraka.
13.Amekuwa toinyo=hanapua.
14.Amekuwa popo=amekuwa kigeugeu
15.Ahadi ni deni=timiza ahadi yako
16.Amewachukua wazee wake=
anawatunza vizuri wazazi
17.Amekuwa mwalimu=yu msemaji sana
18.Amemwaga unga=amefukuzwa kazi 19..Anaulimuwaupanga=anamaneno
makali
20.Ameongeza unga=mepandacheo
21.Agiziarisasi=pigarisasi
22.Kuchungulia kaburi=kunusurika kifo
23..Fyatamkia=nyamaza kimya
24.Fimbo zimemwota mgongoni=ana
alama za mapigo ya fimbo mgongoni
25.Hamadi kibindoni=akibailiyopo
mkononi]
26.Hawapikiki chungu
kimoja=hawapatani kamwe
27.Kupika majungu=kumteta mtu kwa
siri
28.Kumvika mtu kilemba cha ukoka=
umsifu mtu kwa unafiki
29Kula mlungula/kula rushwa=kupokea
rushwa
30.Kupelekwa miyomboni=kutiwa au
kupelekwa jandoni
31.Kujipalia mkaa=ujitia matatani
32.Kumeza au kumezzea mate=utamani
33.Kumuuma mtu sikio=kumnong’oneza
mtu jambo la siri
34.Kumpanyamaya ulimi=
kumdanganya mtu kwa maneno

Visawe na maana zake.

Visawe ni maneno yenye maana sawa.

*Neno=Kisawe*
1. Ardhi=Dunia
2.Ari=Nia
3.Aibu=Soni
4.Azma=Makusudio
5.Binti=Msichana
6.Chakula=Mlo
7.Chanzo=Sababu
8.Cheti=Hati
9.Chuana=Shindana
10.Chubua=Chuna
11.Chubuko=Jeraha
12.Chumvi=Munyu
13.Duara=Mviringo
14.Dunia=Ulimwengu
15.Familia=Kaya
16.Fedha=Hela/Pesa
17.Fukara=Maskini
18.Gari Moshi=Treni
19.Ghasia=Fujo
20.Ghiliba=Hila
21.Godoro=Tandiko
22.Hitimaye=Mwishowe
23.Herufi=Hati
24.Hesabu=Hisabati
25.Hodari=Bingwa
26.Idhini=Ruhusa
27.Jogoo=Jimbi
28.Jokofu=Friji
29.Kandanda=Soka
30.Kenda=Tisa
31.Kichaa=Mwendawazimu
32.Kileo=Pombe
33.Kimada=Hawara
34.Kiranja=Kiongozi
35.Kivumbi=Fujo
36.Kopoa=Zaa
37.Kongoro=Gema
38.Labda=Huenda
39.Labeka!=Abee!/Naam!
40.Laghai=Danganya
41.Lisanj=Ulimi
42.Majira=Wakati
43.Manii=Shahawa
44.Masalia=Mabaki
45.Mashaka=Tabu
46.Mbio=Kasi
47.Mchoyo=Bahili
48.Mdomo=Kinywa
49.Mlolongo=Foleni
50.Motokaa=Gari
51.Msimu=Majira
52.Mtima=Moyo
53.Mtindi=Maziwa Mgando
54.Mtindo=Staili
55.Mtu=Binadamu
56.Muda=Wakati
57.Mvuli=Mvulana
58.Nahodha=Kapteni
59.Nakshi=Urembo
60.Ndoa=Chuo
61.Ndondi=Masumbwi
62.Ndovu=Tembo
63.Nguo=Mavazi
64.Nguzo=Kanuni
65.Nia=Lengo
66.Nuru=Mng’ao
67.Nyanya=Bibi
68.Nyati=Mbogo
69.Ongea=Sema/Zungumza
70.Pombe=Mtindi
71.Raba=Kifutio
72.Rabana=Mola
73.Rafiki=Sahibu/Swahibu
74.Rehani=Poni
75.Rubani=Kapteni
76.Rundika=Tufika
77.Rushwa=Hongo
78.Saka=Winda
79.Sala=Dua
80.Samani=Fanicha
81.Shika=Kamata
82.Shujaa=Jasiri
83.Spika=Kipaza sauti
84.Starehe=Tamasha
85.Sura=Uso
86.Tafrija=Sherehe
87.Terevisheni=Runinga
88.Thenashara=Kumi na mbili
89.Tumbiri=Ngedere
90.Ugonjwa=Maradhi
91.Uja=Ubinadamu
92.Ukaidi=Ujeuri
93.Ukumbi=Surua
94.Ukuta=Kiambaza
95.Ukwasi=Utajiri
96.Upara=Kidazi
97.Urembo=Umaridadi
98.Vamio=Shambulio
99.Vifijo=Vigelegele
100.Vunja=Pasua
101.Vurugu=Fujo
102.Vuu=Ghafla
103.Nyema=Vizuri
104.Wajihi=Uso
105.Wakala=Ajenti
106.Waraka=Barua
107.Waza=Fikiri
108.Weupe=Mwangaza
109.Weusi=Giza
110.Wiki=Juma
111.Winda=Nepi
112.Wivu=Husuda
113.Chupi=Kocho
114.Karai=Beseni/Dishi
115.Mamba=Kenge.

Mbona nisirudi.

Natamani nikarudi, siku zile zamani
Ila tu imenibidi, uwezo sina sinani
Nami ningejitahidi, pale ninapotamani
Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma?
#
Natamani zama zile, zisokuwa na potole
Lipopiga ukelele, nihudumiwe wavyele
Ya kesho nisiyaole, vya shubiri nisivile
Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma?
#
Mambo ya kukosa kazi, katu nisiyaelewe
Kodi ikawe upuzi, nisikie kwa wenyewe
Sinao hata mchuzi, nyumba nje kafungiwe
Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma?
#
Lakini ningejipanga, kuyafanya maamuzi
Singekuwa tena bunga, nikashinde kwa upuzi
Kuovu singejiunga, ningeenda na wajuzi
Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma?
#
Ningeepuka ushenzi, na kuwinga kwa ukali
Nikijua hilo penzi, kamwe haliwi ugali
Kwangu ngekuwa mlinzi, nikaishi kisahili
Ila sasa nifanyeje, jua litarudi nyuma?
#

(Mlumbi Mtafumaniwa Okelo)

Chelsea yamsajili Kai Havertz.

Mashabiki wa klabu ya Chelsea inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza wana kila sababu ya kutabasamu baada ya usajili wa kiungo matata.Kai Havertez ambaye alikuwa mchezaji wa Bayern Leverkusen amedhibitishwa kusajili na ‘the blues”.

Inadaiwa kuwa amekubali mkataba wa miaka mitano na klabu hiyo.Habari hizi zinatokana na kauli ya Fabrizio Romano kwenye mtandao wa kijamii alipoulizwa na shabiki mmoja kama usajili huo umekamilika.

Usajili huu unakuja siku chache tu baada ya klabu hiyo kuwasajili wachezaji Hakim Ziyech,Timo Werner,Thiago Silva na Malang’ Sarr.